My Blog List

Saturday, March 17, 2012

CHADEMA MKURANGA YAZIDI KUSOMBA WASOMI

Na Nova Kambota,
16 March, 2012

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Mkuranga kimezidi

kujiongezea umaarufu wake kwa kuzidi kusomba wasomi wengi wilayani
humo. Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mkuranga Bw Jamal Lwei
amekaririwa akisema...kwetu haya ni mafanikio makubwa kwani chama sasa
kinakua kwa kasi na wasomi wanaonekana kukubali mipango, sera na
harakati zetu....

Mwenyekiti huyo aliyasema hayo mapema leo asubuhi huku pia akitoa

salamu za pole kwa baadhi ya wanamkuranga waliofikwa na maafa kutokana
na mvua zilizoambatana na upepo siku ya jana , ambapo taarifa za awali
zinabainishwa kuezuliwa kwa mapaa ya baadhi ya nyumba za wananchi wa
wilaya hiyo na nyingine kuangukiw na miti.

Mwenyekiti huyo pamoja na mambo mengine pia amezungumzia uchaguzi wa

Arumeru Mashariki huku akisisitiza kuwa ana imani wana Arumeru
watamchagua Nassari kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusimamia sera za
kimaendeleo.

Duru za kisiasa kutoka jimbo la Mkuranga ambalo linashikiliwa na Adam

Malima zinabainisha kuwa sababu ya wasomi wengi kuhamia CHADEMA ni
pamoja na kushindwa kwa sera za CCM za maisha bora kwa kila mtanzania
huku wananchi wakiendelea kusota kwenye umasikini mkubwa huku viongozi
wa serikali hasa wale wateule wa rais Kikwete wakiogelea kwenye
utajiri mkubwa. 

Baadhi ya wananchi wameenda mbali zaidi huku wakihoji
kuhusu mgao wa umeme, matokeo mabovu ya shule za sekondari na msingi
pamoja na huku wakiishinikiza serikali iwalipe malipo ya fedha za
korosho ambazo wamesema bado hawajalipwa.
Reactions::

Friday, March 2, 2012

UCHUMI NA MAENDELEO


WATOTO WA KIKE WAJENGEWE UWEZO WA KUMUDU MAISHA.


Hali ya sasa ya watoto wa kike hasa waishio maeneo ya vijijini kwa walio wengi wanatoka katika familia zenye kipato cha chini na asilimia kubwa wana uwezo wa kiakili kwa maana ya uwezo wa kumudu masomo ya darasani lakini wakifikia kuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari hapo ndipo kunakuwepo na ugumu.

Hali ya kipato cha wazazi cha kumpeleka mtoto wa kike shule inashindikana kiasi cha kumkatisha tamaa na kumfanya ajiingize kwenye vishawishi vingine na hivyo ili kuondoa tatizo hili katika  jamii yetu ya Kitanzania,kunahitajika jitihada za pamoja za Serikali,Taasisi mbali mbali na wadau wa Maendeleo wawe na dhamira ya kweli na matumizi sahihi za raslimali zilizopo.

Serikali na wadau wa maendeleo na jamii kwa ujumla inabidi kuwabaini watoto wa kike ambao wako katika Mazingira hatarishi kwa sababu ya umaskini wa familia zao wameshindwa kupata haki zao za msingi na kwamba wakiwabaini wataweza kuwalipia karo na mahitaji mengineyo ya shule.